Hadija ninakuita, naomba uniitike
Kukupenda sitosita, hata kinipiga teke
Nilini n’takupata, nikuite wangu mke
Penzi ni kama kohozi, kulificha sitoweza
Ni weye nishaamua, mwengine sitompenda
Kila mtu kwa mtaa, yuajua nakupenda
Kupitiya i sanaa, naapa sitokutenda
Penzi ni kama kohozi, kulificha sitoweza
Alokupa u urembo, kakupa pia tabia
Sitoboi yote mambo, mengineyo takwambia
Linaua hilo umbo, bayana nawaambia
Penzi ni kama kohozi, kulificha sitoweza
Niurumie nakuomba, moyo upate tulia
Tuianze yetu nyumba, daima kufuraia
Tumshukuru Muumba, aweze kutujalia
Penzi ni kama kohozi, kulificha sitoweza
Naakika tanikithi, na jina langu ni hili
Kaburu wa Kariithi, Aderea ndo la pili
Mtungaji mwenye haathi, nayependa wana wali
Penzi ni kama kohozi, kulificha sitoweza
Great poet in the making.Do me a favour and please maintain your posts in Kiswahili,I like!:-)
ReplyDeleteGreatly humbled Balla,I promise to n thnx alot
ReplyDeleteLisilo budi hubidi, ewe wa Kariithi
ReplyDeleteFanya hala bisha hodi,takukubali amini.
Akufae maishani, hadi pale kaburini
Penzi ni kama sukari, limung'unye kwa ulimi.